Breaking News

Conte achukizwa na kinachoendelea Chelsea

Kulikuwa na taarifa kwamba kocha Antonio Conte hakuwa na furaha kuhusu jinsi klabu ya Chelsea inavyoendeshwa na aliwaza kutoongeza mkataba katika klabu hiyo.

Baadaye taarifa za Conte kuchoshwa na Chelsea zikazimwa na tukaambiwa kocha huyo ana furaha na Chelsea na ataendelea kukinoa kikosi hicho cha The Blues.

Baadae jipya likaibuka ikiwa ni ugomvi kati ya Conte na mshambuliaji Diego Costa kwa kile kinachosemwa kwamba Conte alimuambia Costa kwamba hamhitaji katika msimu ujao wa ligi.

Baada ya Conte kusema hamtaki Costa akahamishia majeshi Romelu Lukaku ambaye alionekana mtu sahihi kuziba nafasi ya Costa na kutaka klabu imnunue.

Lakini wiki hii hali imezidi kumchafukia Conte kwani taarifa zinadai mshambuliaji huyo wa Everton yuko njiani kujiunga na mashetani wekundu wa Manchester United.

Taarifa zinadai Conte amechukizwa sana na jambo hilo na anaona kama viongozi wanamfanya ashindwe kufikia malengo yake na hili linfanya awaze kuondoka.

Conte inasemekana tangu kuisha kwa ligi kuu Uingereza amekuwa mpole sana huku akikosa furaha kwa jinsi dirisha la usajili linavyoendeshwa na klabu hiyo.

Lakini pamoja na hayo kuna taarifa zimetoka kwamba klabu hiyo imeamua kupambana kuhusu Lukaku na tayari wametuma ofa Everton kujaribu kuwapiku Manchester United kumnunua mchezaji huyo.

Endapo Chelsea watamkosa Lukaku itawabidi waanze upya kutafuta mtu wa kuziba pengo la Diego Costa au pengine Conte anaweza kukaa chini na kumalizana na Costa.

No comments