Madhara unayoweza kuyapata kwa kuanika nguo ndani
Watu wengi hupenda kuanika nguo ndani baada ya kuzifua hasa pale wanapodhani kuanika nje ni hatari kwa kuhofia wizi au mvua bila kujua madhara wanayoyapata kutokana na kuanika nguo ndani.
Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha New South Wales Australia wamegundua madhara yanayotokana na kuanika nguo ndani ambayo ni pamoja na kusababisha ugonjwa wa pumu na matatizo ya mapafu.
Wataalam hao wanadai kuanika nguo ndani kunasababisha bakteria ambao hushambulia mfumo wa upumuaji kujikusanya kwenye nguo mbichi iliyoanikwa ndani kuliko nguo iliyoanikwa nje kwa sababu bakteria hao hawakai nje kwenye jua.
Akizungumza na KidSport mmoja wa wataalamu hao Dr. Christine Cowiealisema bakteria wengi wanaosababisha ugonjwa wa pumu hupatikana ndani ya nyumba na hupendelea hali ya unyevunyevu hivyo mtu anapovaa nguo iliyoanikwa ndani hata ikiwa imekauka anaweza kupata ugonjwa wa pumu.
No comments