Jokate amwaga misaada
Mwanamitindo Jokate Mwegelo
Dar es Salaam. Mwanamitindo Jokate Mwegelo leo Ijumaa ametoa zawadi za Eid katika kituo cha yatima na wajane cha Ahbaabul Khairiya kilichopo Mwananyamala B, jijini Dar es Salaam.
Katika zawadi hizo Jokate alitoa mchele kilo 250, unga kilo 250, mafuta ya kupikia, mbuzi wawili na nguzo za watoto na wanawake.
Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo, Jokate ambaye mwaka 2006 alishika nafasi ya pili katika Shindano la Miss Tanzania, amesema ameguswa kuwasaidia watu wenye uhitaji ili nao washerehekee Sikukuu ya Eid kwa furaha.
"Nikiwa kama mwanajamii nimeguswa na watoto hawa na akina mama nikaona si vibaya nikajikusanya na kutoa kidogo nilichonacho ili nao wafurahie sikukuu."
Mkuu wa kituo hicho, Ahmed Shebe ameshukuru kwa msaada huo na kuwataka wasanii wengine kuiga mfano huo.
"Ukiwasaidia wasiokuwa na uwezo Mungu anakuongezea maradufu, niwasihi wasanii kujitoa kwa ajili ya wanajamii na si kufanya matendo na matumizi ya anasa,"amesema Shebe.
No comments