Fanya hivi kujichunguza kama una saratani ya matiti ( BREAST CANCER )
Saratani ya matiti imekua ikiwatesa wanawake wengi kutokana na dalili zake kutoonekana mapema na pia wakati mwingine hali hii hutokea kwa sababu hawana tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara na kupeleke kugundulika kua wana saratani ikiwa ugonjwa huo upo katika hali mbaya (late stage) Kumbuka kujichunguza ndio njia bora ya kugundua saratani ikiwa bado ndogo, na una weza kujichunguza mara 2 au tatu kila mwezi.
Zifuatazo ni hatua tano muhimu katika kujichunguza kama una satratani ya matiti.
HATUA YA KWANZA
Simama mbele ya kioo mkono mmoja weka pembeni na angalia kama kuna mabadiliko yeyote kama vile uvimbe ,kovu,au matokwa yeyote kwenye chuchu.
HATUA YA PILI
Angalia kama kuna mabadiliko yeyote kwenye mistari ya kontua ya matiti
HATUA YA TATU
Minya chuchu taratibu kama kuna uchafu wowote unao toka
HATUA YA NNE
Lala kitandani kwa mgongo, weka mkono mmoja nyuma ya kichwa, papasa kwa kutumia mkono mwingine. Anza na papasa kwa mizunguko midogo midogo na uhisi kama kuna uvimbe wowote ama maumivu.
HATUA YA TANO
Rudia hatua ya nne kwa upande mwingine wa titi.
Kama utaona dalili zozote usizo zielewa ni vyema kumuona daktari kwa vipimo na ushauri zaidi.
kumbuka kua kujichunguza mwenyewe sio mbadala wala hakuzuii wewe kumuona daktari kwa ushauri na uchunguzi zaidi.
Mungu akubariki sana kwa elimu hii muhimu sana kwetu wanawake. Hakuna Nyumba ilyokosa mwanamke.Kama bibi na mama hawapo yopo make, Dada au shangazi.nitawajuza wengine kwa kadri nitakavyojaaliwa.Asante sana
ReplyDelete