Breaking News

Exclusive: Okwi atua  Msimbazi kuziba pengo la Ajib


Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi 25 msimu ujao.

Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, ametua Bongo jana usiku na leo mchana nilipata nafasi ya kuzungumza na amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Simba. 

“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi.

Okwi na akiwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hans PopeUpdates: Muda mfupi uliopita, klabu ya Simba kupitia msemaji wao Haji Manara wamethibitsha Okwi amemwaga wino wa kuitumikia Simba, mkatabawa miaka miwili. 

No comments