Breaking News

UPDATE: Malima afikishwa Mahakamani baada ya Polisi kufyetua risasi

Jana May 15, 2017 ilisambaa video ikimuonesha aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha kwenye awamu ya nne, Adam Malima akizozana na Askari Polisi kwa kilichoelezwa kuwa ni baada ya dereva wa kiongozi huyo kupaki gari sehemu isiyotakiwa.

Tukio hilo lilipelekea Askari kumtaka dereva wa kiongozi huyo kupeleka gari kwenye Yard ya kampuni moja inayosimamia sheria za barabarani ambapo ilielezwa kuwa dereva alikataa kutii hivyo ikaibua majibizano.
Leo May 16, 2017 Kiongozi huyo amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ikiwemo kumzuia Askari kutekeleza majukumu yake ya kazi ambapo hata hivyo, Malima ameachiwa kwa dhamana ya Shilingi Milioni 5.

Naibu Waziri wa Fedha wa zamani Adam Malima amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kumzuia askari kufanya kazi, ameachiwa kwa dhamana ya Mil 5.
pic.twitter.com/8AdSVASFa0

No comments