Breaking News

MALI KUIBUKA NA USHINDI fainal za AFCON

May 28 2017 mchezo wa fainali ya AFCON U-17kati ya Mali Mabingwa watetezi dhidi ya Ghanaulichezwa katika uwanja wa Stade Amitie LibrevilleGabon, huo ukiwa ni mchezo uliyokuwa unatajwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na viwango vya timu hizo mbili.

Usiku wa May 28 2017 kwa mara nyingine tena Maliwanatwaa Ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kufanikiwa kuifunga Ghanagoli 1-0, goli la Mali lilifungwa na Mamadou Samakekwa mkwaju wa penati dakika ya 23.

Tanzania inakuwa timu pekee ambayo haijawahi kuruhusu goli katika mchezo dhidi ya Mali katika michuano ya AFCON U-17 toka Mali atwae taji hilo mwaka 2015 nchini NigerMali katika michuano yaAFCON iliyofanyika Niger 2015 alitoka sare moja tu ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya South Africa na katika michuano hii Tanzania ndio haijafungwa.

Mali bado wanaendelea kuwa na timu imara ya vijana chini ya umri wa miaka 17, baada ya mchezo huo katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwaalikabidhiwa bendera na Rais wa CAF Ahmad Ahmad kama ishara ya kuipa Tanzania uenyeji wa michuano ya AFCON U-17 mwaka 2019.

Salam

Rais wa CAF Ahmad Ahmad akiwakabidhi Kombe Mali

Rais wa CAF Ahmad Ahmad akimvalisha medali ya Ubingwa mchezaji wa Malia

Ghana ambao ni washindi wa pili wa AFCON U-17

Guinea baada ya kupewa medali za mshindi wa tatu kwa kuifunga Niger

No comments