Leo ni Leo Nay wa Mitego, Barnaba Kukinukisha Dar Live
Nay wa Mitego akiwarusha roho mashabiki katika Viwanja vya Karume jana.
BAADA ya kuliamsha dude katika shoo ya bure jana ndani ya Viwanja vya Karume jijini Dar, Mkali wa Ngoma ya Wapo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anatarajiwa kuungana na mastaa kibao katika bonge la shoo linalotambulika kama Wapo Concert leo (Mei 20), ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Nay alianza kwa kuwapongeza mashabiki wote waliofurika jana katika Viwanja vya Karume na kuwasihi moto uendelee kuwa huohuo siku ya leo wajitokeze kwa wingi.
“Nimefarijika sana, vijana wengi bado wanatamani burudani kutoka kwangu na leo (jana) ile ilikuwa rasharasha tu mvua ya mawe ipo kesho (leo) ndani ya Dar Live.
“Kwa zaidi ya miaka mitatu sijafanya shoo ya kishindo na safari hii itakuwa kiboko maana nimejiandaa vya kutosha kuwapa mashabiki kitu wanachopenda.
Nitapiga ngoma zote kuanzia Itafahamika, Helo, Muziki Gani, Muda Wetu, Pale Kati Patamu, Uko Kwenu Vipi hadi Shika Adabu Yako na Wapo,” alisema Nay.
Naye Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliongezea kuwa usiku huo unaotambulika pia kama Usiku wa Wabishi, watakuwepo wakali kibao wanaotikisa katika vichekesho na Muziki wa Bongo Fleva.
Kala Jeremiah
“Tutakuwa na mabingwa wa vichekesho wanaotikisa kwa sasa Bongo, Mkali Wenu na Ebitoke, tutakuwa pia na Shilole wengi mmezoea kumuita Shishi ambapo atakamua ngoma zake kibao bila kusahau inayobamba kwa sasa ya Hatutoi Kiki, atakuwepo pia Barnaba Classic, wengi mnamtambua kwa sauti tamu aliyonayo, basi atawaburudisha kwa ngoma zake nyingi ikiwemo Milele, Magumegume, Lover Boy, Nakutunza, Mapenzini na Lonely huku pia mkali mwingine Kala Jeremiah akitinga na ngoma zake kali kama Dear God, Waambieni, Usikate
Tamaa na Wana Ndoto,” alisema Mbizo na kuongezea; “Mashabiki wasiwaze kabisa kuhusu kiingilio kwani lengo ni kutoa shoo sawa na bure hivyo watalipia hela ya mboga yaani kiingilio kiduuuuuchu sana cha shilingi 5,000 tu kitakachomuwezesha kila mpenda burudani aweze kuhudhuria na kuimba Wapo pamoja na Nay jukwaa moja,” alimaliza Mbizo.
No comments