JINSI YA KURUDISHA DATA ZAKO ZILIZOPOTEA KWENYE SIMU
Njia Za Kupata Data Zako Zilizopotea (Zilizofutwa) Katika Kifaa Cha Android!
Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, TeknoKona inakuletea njia.
Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye
• Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako
• Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) yanayofanyikaga automatiki yasifanyike. Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua
Tuifahamu Njia
Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi
Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha kompyuta yako na simu kwa kutumia USB. Kuna baadhi ya matoleo ya vifaa vya android, ukichomeka USB katika kompyuta haijionyesha katika mfumo ule wa ‘kuonekana kama umechomeka Flash tuu’ .
Kama simu yako haifanyi hivyo na una uhakika taarifa zako hizo zilikuwa katika sehemu ya memory kadi unaweza ukatumia adapta ya memori kadi hiyo na kuichomeka katika kompyuta ili isome mafaili yaliyomo ndani.
Sasa unaweza ukashusha programu ya Recuva katika kompyuta (Unaweza ukashusha ya bure au ya kulipia)
Bofya hapa Kushusha Recuva
Ukishafungua Recuva kitu cha kwanza ni kuchagua mafaili gani unayotaka kuyafufua katika kifaa chako (picha, video n.k). Unaweza ukachagua sehemu husika ambapo unataka mafaili ya eneo hilo yafufuliwe. Kitu cha muhimu cha kuweka akilini hapa ni kwamba program ya Recuva itaonyesha maeneo ambayo inaweza fufua mafaili yaliyofutika tuu.
Mpaka hapo nadahani umekuwa mtaalamu juu ya jambo la kufufua vitu eeeeh? (haha!). Fufua vitu vyako vya muhimu pindi tuu vinavyofutika kwa bahati mbaya.
Kwa kutumia njia hii huweza ukawa na wasiwasi kuwa utakuja kupoteza vitu vyako na usivipate tena. Kama ukijitokeza hivyo unatumia Recuva tuu.
No comments